Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika matendo...
Sahihi
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na mi...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayezua katika dini yetu hii, yale yasiyok...
Sahihi
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetunga au kubuni jambo katika dini au akafanya amali yoyote ambayo haikuelekezwa na dalil...
Imepokewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja tukiwa tumekaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ghaf...
Sahihi
Imepokelewa na Imamu Muslim

Anaeleza Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Jibrili -Amani iwe juu yake- alijitokeza kwa Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- kw...
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Umejen...
Sahihi
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ameufananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Uislamu na jengo madhubuti kwa nguzo zake tano zenye kulibeba jengo hilo, na mambo mengine ya Uisl...
Kutoka kwa Muadhi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa nimepanda Punda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Punda akiitw...
Sahihi
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Anaziweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa haki za Mwenyez...

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yote huzingatiwa nia, na hukumu hii ni ya ujumla katika amali zote, kwanzia ibada na miamala, atakaye kusudia kupata masilahi katika amali yake hatopata zaidi ya masilahi na wala hatopata thawabu, na atakayekusudia katika amali yake kujiweka karibu na Allah Mtukufu, atapata thawabu na malipo kupitia amali yake hata kama litakuwa ni jambo la kawaida, kama kula na kunywa. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.
Hadeeth details

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetunga au kubuni jambo katika dini au akafanya amali yoyote ambayo haikuelekezwa na dalili yoyote kutoka katika Qur'ani na Sunna, basi jambo hilo litarejeshwa kwa mfanyaji wake na halitokubaliwa mbele ya Allah.
Hadeeth details

Anaeleza Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Jibrili -Amani iwe juu yake- alijitokeza kwa Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- kwa sura ya mtu asiyejulikana, na miongoni mwa sifa zake nikuwa, nguo zake ni nyeupe mno, na nywele zake ni nyeusi mno, haonekani kuwa na athari za safari ikiwemo kuonyesha uchovu, vumbi, na nywele kutimka, na nguo kuchafuka, na hakuna yeyote amjuaye katika wote waliopo, nao wakiwa wamekaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akakaa mbele ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkao wa mwanafunzi, akamuuliza kuhusu Uislamu, akamjibu kwa nguzo hizi ambazo zimeambatana na kukiri shahada mbili, na kudumu na sala tano, na kutimiza zaka kwa wastahiki wake, na kufunga mwezi wa Ramadhani, na kutekeleza faradhi ya Hija kwa mwenye uwezo. Muulizaji akasema: Sadakta!, Masahaba wakashangaa kwa swali lake la kuonyesha kuwa hajui kitu kwa muonekano wake, kisha anamsadikisha!. Kisha akamuuliza kuhusu imani, akamjibu kwa nguzo hizi sita zilizokusanya kuamini uwepo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa zake, na kumpwekesha kwa vitendo vyake kama kuumba, na kumpwekesha kwa ibada, nakuwa Malaika aliowaumba Allah kwa nuru ni waja waliotukuzwa hawamuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na amri yake ndio wanayoifanyia kazi, na kuamini vitabu vilivyoteremshwa kwa Mitume kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama Qur'ani na Taurati na Injili na vinginevyo, na kuwaamini Mitume wenye kumfikishia Mwenyezi Mungu dini yake, miongoni mwao ni Nuhu na Ibrahim, na Mussa, na Issa, na wa mwisho wao ni Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yao wote- na wengineo katika Manabii na Mitume, na kuamini siku ya mwisho, na yanaingia hapa maisha baada ya kifo ikiwemo kaburi na maisha ya barzakh (Akhera), na kuamini kuwa Mwenyezi Mungu amekadiria mambo kulingana na ujuzi wake uliotangulia na hekima zake zikapelekea hivyo, na kuyaandika kwake, na matashi yake kwa mambo hayo, na kutokea kwake kwa namna aliyoikadiria Mwenyezi Mungu, na kuviumba kwake. Kisha akamuuliza kuhusu Ihisani, akamueleza kuwa Ihisani ni amuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba anamuona, ikiwa hatoweza kufikia daraja hili basi amuabudu Allah kana kwamba Allah anamshuhudia, daraja bora zaidi kushuhudiwa, na ndio ya juu zaidi, na ya pili ni daraja ya kuchunga (Kuleta hisia kua unamuona mbele yako). Kisha akamuuliza Kiyama ni lini? Akabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa elimu ya Kiyama ni katika elimu alizobaki nazo Mwenyezi Mungu ujuzi wake, hawezi kuijua yeyote katika viumbe, si muulizaji wala muulizwaji. Kisha akamuuliza kuhusu alama za Kiyama? Akabainisha kuwa miongoni mwa alama zake ni kukithiri kwa wajakazi (Masuria) na watoto wao, au ni wingi wa watoto kutowatii mama zao, kiasi cha kuishi nao kama watumwa wao, nakuwa wachunga mbuzi na masikini watakunjuliwa dunia katika zama za mwisho, na watafaharishana katika kuremba majengo na kuyarefusha. Kisha akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muulizaji ni Jibril alikuja kuwafundisha Masahaba dini tukufu.
Hadeeth details

Ameufananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Uislamu na jengo madhubuti kwa nguzo zake tano zenye kulibeba jengo hilo, na mambo mengine ya Uislamu kama nyenzo zenye kulikamilisha jengo hilo, Na nguzo ya kwanza katika nguzo hizo ni: Shahada mbili; Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hizo mbili ni nguzo moja; kila moja haitengani na nyingine, mja anazitamka kwa kukiri umoja wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa yeye pekee pasina mwingine, na kufanyia kazi makusudio ya nguzo hii, na kwa kuamini utume wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumfuata yeye. Na nguzo ya pili: Ni kusimamisha swala, nazo ni swala tano za faradhi usiku na mchana: Alfajiri, Adhuhuri, lasiri, Maghribi, na Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Na nguzo ya tatu: Ni kutoa zaka ya lazima, nayo ni ibada ya mali ya wajibu katika kila mali iliyofikia kiwango maalumu katika sheria, ambayo hupewa wastahiki wake. Na nguzo ya nne: Ni Hija, nayo nikutia nia ya kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada, kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. Na nguzo ya tano: Ni kufunga mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na vinginevyo miongoni mwa vyenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama jua.
Hadeeth details

Anaziweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haki za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na haki za waja kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa haki za Mwenyezi Mungu kwa waja ni kuwa wamuabudu yeye peke yake na wala wasimshirikishe yeye na kitu chochote. Na kuwa haki za waja kwa Mwenyezi Mungu ni kutowaadhibu wenye kumpwekesha ambao hawamshirikishi yeye na chochote. Kisha Muadhi akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hivi kwa nini nisiwape watu habari hii njema ili wafurahi kwa jambo hili bora? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamkataza kwa kuogopea kuwa watategemea habari hiyo.
Hadeeth details

Alikuwa Muadhi bin Jabali -Radhi za Allah ziwe juu yake- amepanda nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya mnyama wake, akamuita: Ewe Muadhi? Akarudia wito mara tatu; Kwa kusisitiza umuhimu wa yale atakayomueleza. Na mara zote hizo Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akimjibu kwa kusema: "Labaika kwa heshima yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Yaani: Nimekujibu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu jibu moja moja, na ninataka utukufu kwa kukujibu wewe. Akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa hakuna yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuaubudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isopokuwa Allah, na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa ukweli toka moyoni mwake, si muongo, ikiwa atakufa katika hali hii basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni. Muadhi -Radhi za Allah ziwe juu yake- akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- awaeleze watu ili wafurahi na wajipe bishara njema? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akachelea watu kubweteka katika hilo, na wapunguze kufanya matendo. Muadhi hakumsimulia hilo yeyote ila kabla ya kifo chake; kwa kuhofia kuingia katika dhambi za kuficha elimu.
Hadeeth details

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesema na akashuhudia kwa ulimi wake yakuwa "Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu", Yaani: Hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na akayakanusha yote yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na akajitenga na dini zote isipokuwa Uislamu, itakuwa haramu mali yake na damu yake kwa muislamu, hatumiliki isipokuwa dhahiri katika matendo yake, hapokonywi mali yake na wala haimwagwi damu yake, isipokuwa atakapofanya uhalifu au jinai linalopelekea hivyo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu. Na Allah atasimamia hesabu yake siku ya Kiyama, akiwa ni mkweli atamlipa, na akiwa mnafiki atamuadhibu.
Hadeeth details

Mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo mawili: ambayo yanasababisha kuingia peponi na yanayo sababisha kuingia motoni? Basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akamjibu kuwa mambo ambayo yanamsababishia mtu kupata pepo ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na wala hamshirikishi na kitu chochote. na kuwa mambo ambayo yanapelekea kuingia motoni, ni kuwa afe mtu hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na anamuwekea Mwenyezi Mungu washirika na vifananishwa katika uungu wake na uumbaji wake na katika majina yake na sifa zake.
Hadeeth details

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeelekeza chochote katika vile ambavyo vinapasa kuwa vya Mwenyezi Mungu pekee kwa asiyekuwa yeye, kama kumuomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutaka msaada kwa asiyekuwa yeye, na akafa katika hali hiyo basi huyu ni katika watu wa motoni. Na akaongeza bin Masuod radhi za Allah ziwe juu yake kuwa atakayekufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika pepo.
Hadeeth details

Alipomtuma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Muadhi Ibn Jabal -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwenda katika miji ya Yemen kama mlinganizi wa kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu na kama mwalimu, alimuweka wazi kuwa atakumbana na jamii ya Wakristo; ili awe na maandalizi, kisha aanze katika kuwaita kwake na mambo muhimu zaidi kisha yanayofuatia, Atawaita kurekebisha itikadi kwanza; washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; Kwa sababu wao kwa itikadi hiyo yakuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake; wataingia katika Uislamu, ikiwa watatii hilo basi awaamrishe wasimamishe swala; kwani huo ndio wajibu mkubwa baada ya tauhidi, Watakapoisimamisha awaamrishe matajiri wao kutoa zaka ya mali zao kuwapa mafukara wao, kisha akamtahadharisha na kuchukua mali bora; kwa sababu ya wajibu ni mali ya kati na kati, Kisha akamuusia aiepuke dhulma; asijekumuombewa dua mbaya aliyemdhulumu, kwani dua yake hupokelewa.
Hadeeth details

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mtu mwenye furaha zaidi kuliko wote kwa uombezi wake siku ya Kiyama ni yule atakayesema: "Laa ilaaha illa llaah kwa kutakasa nia toka moyoni mwake" Yaani: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na asalimike na ushirikina na riyaa(kufanya mambo kwa kujionesha).
Hadeeth details

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa imani ina sehemu moja pamoja na mambo mengi, yanakusanya matendo itikadi na kauli. Nakuwa jambo la juu zaidi katika mambo ya imani ni kauli ya: Laa ilaaha illa llaah", kwa kujua maana yake, na kufanyia kazi matakwa yake, yakuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola Mlezi Mmoja wa pekee mwenye kustahaki kuabudiwa peke yake pasina mwingine zaidi yake. Nakuwa tendo dogo kabisa katika matendo ya imani ni kila chenye kuwaudhi watu katika njia zao. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa haya ni katika mambo ya imani, nayo ni tabia inayomsukuma mtu kufanya mazuri na kuacha mabaya.
Hadeeth details