Na timizeni Hija na Umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa mkizuiwa,basi (chinjeni) wanyama walio wepesi kupatikana. Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjoni mwao. Na atakaye kuwa mgonjwa au ana vya kumuudhi kichwani mwake basi atoe fidiya kwa kufunga au kwa kutoa sadaka au kuchinja wanyama. Na mtakapo kuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanya Umra kisha ndio akahiji, basi achinje mnyama aliye mwepesi kumpata. Na asiye pata, afunge siku tatu katika Hija na siku saba mtakapo rudi; hizi ni kumi kaamili. Hayo ni kwa ajili ya yule ambaye watu wake hawako karibu na Msikiti Mtakatifu. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
[سورة البقرة
] • 196
Hao ndio watakao pata sehemu yao kwa sababu ya yale waliyo yachuma. Na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
[سورة البقرة
] • 202
Nyinyi mmehalalishiwa kuvua vinyama vya baharini na kuvila, kwa faida yenu na kwa wasafiri. Na mmeharimishiwa mawindo ya wanyama wa bara maadamu mmeharimia Hija. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mtakusanywa kwake.
[سورة المائدة
] • 96
Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji na kuamirisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
[سورة التوبة
] • 19
Kisha wajisafishe taka zao, na waondoe nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Aufaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah, Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati wamil al Ardhwi wamil amaashi ita min shai in ba'ad".
Sahihi
Imepokelewa na Imamu Muslim
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja nyakati za usiku nilimkosa kitandani Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikaanza kumtafuta ukaangukia mkono wangu ndani ya nyayo zake zikiwa zimesimamishwa akiwa ndani ya msikiti, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako"
Sahihi
Imepokelewa na Imamu Muslim
Imepokelewa kutoka kwa Ubaiyya bin Kaab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi kwako?" Akasema: Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi. Akasema: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir."
Sahihi
Imepokelewa na Imamu Muslim
Kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake na alikuwa kapigana vita pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- takriban vita kumi na mbili (12) anasema: Nilisikia mambo manne kutoka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, yakanifurahisha sana, anasema: "Asisafiri mwanamke mwendo wa siku mbili mpaka awe pamoja na mume wake, au maharimu yake (Ndugu asiyeweza kumuoa), hakuna kufunga ndani ya siku mbili: Idil Fitri na Idil Adh-ha, na hakuna swala baada swala ya Asubuhi mpaka lichomoze jua, na wala baada ya Lasiri mpaka lizame, na wala haifungwi safari isipokuwa katika misikiti mitatu: Msikiti mtukufu (wa Makka), na Msikiti wa Aqswa (Palestina), na msikiti wangu huu (Madina)".
Sahihi
Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu amesema: Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake, na akawa bado mja wangu anaendelea kujiweka karibu yangu kwa ibada za sunna (zisizokuwa za lazima) mpaka nitafikia mahala nitampenda, nikishampenda: Nitakuwa sikio lake analosikilizia, na jicho lake analotazamia, na mkono wake anaoshikia, na mguu wake anaotembelea, na hata akiniomba hakika nitampa, na hata akinitaka kinga hakika nitamlinda, na sijawahi kusita katika jambo lolote ninalotaka kulifanya kama kusita kwangu katika (kuitoa) nafsi ya muumini, hapendi kufa na mimi sipendi kumuudhi".